• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China aanza ziara rasmi nchini Ufaransa

    (GMT+08:00) 2019-03-26 14:44:24

    Baada ya miaka mitano, rais Xi Jinping wa China amewasili tena mjini Paris na kuanza ziara rasmi nchini Ufaransa.

    Ziara hiyo imekuja katika wakati maalumu ambapo China na Ufaransa zinaadhimisha miaka ya 55 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi na miaka 100 ya Harakati ya Vijana wa China kwenda kusoma nchini Ufaransa. Rais Xi amesema amekuja akiwa na hisia maalumu kwa watu wa Ufaransa, na atashirikiana na upande wa Ufaransa katika kuota mizizi ya matumaini mapya ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

    Jumapili usiku, rais Xi Jinping na mke wake Bibi Peng Liyuan walihudhuria tafrija binafsi iliyoandaliwa na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na mke wake kwenye nyumba yao ya Villa Kerylos mjini Nice, na walifanya mazungumzo kwa muda wa zaidi ya masaa matatu.

    Jumatatu, marais hao wawili walikutana tena na kufanya mazungumzo kwa masaa matano, ambapo marais hao wamekubaliana kwa kauli moja kuwa China na Ufaransa zitajenga uhusiano wa wenzi wa kimkakati ulio imara na mwenye nguvu katika mwanzo mpya wa kihistoria.

    Mwaka 1964, Ufaransa ilikuwa ni moja ya nchi za kwanza za magharibi kuanzisha uhsuiano wa kibalozi na China. China na Ufaransa zina mitizamo inayofanana kuhusu siasa za kimataifa, hali inayotoa msukumo mkubwa kwa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Safari hii, viongozi wa China na Ufaransa pia wameweka mpango wa kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika zama mpya, haswa kwenye nyanja za kuinua kiwango cha kuaminiana kisiasa, ushirikiano wa kiutendaji na mawasiliano ya kiutamaduni.

    Jana, marais wa China na Ufaransa walishuhudia kusainiwa kwa makubaliano 14 ya ushirikiano kati ya pande mbili. Imefahamika kuwa China na Ufaransa pia zimesaini makubaliano ya kibiashara yenye thamani ya Euro bilioni kumi, na kuamua kushirikiana kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Rais Xi Jinping amesema, sheria ya uwekezaji wa nje ya China iliyotolewa hivi karibuni itaendelea kupunguza vizuizi vya kuingia katika soko la China, kuboresha mazingira ya kibiashara, kuimarisha ulinzi wa hakimiliki na kujenga hali mpya ya ufunguaji mlango kwa nje.

    Rais Xi amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na Ufaransa katika kutoa mchango mkubwa zaidi wa kihistoria kwa ajili ya kujenga dunia iliyo shirikishi na safi, na yenye amani, usalama na ustawi wa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako