• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tani 6,000 za muhogo kuzalishwa Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-03-26 18:49:39

    Jumla ya tani 6,000 za unga wa muhogo zinatarajiwa kuzalishwa kwa mwaka na kiwanda cha kisasa cha kuzalisha bidhaa hiyo kwa mwaka. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ulimaji na Usindikaji muhogo ijulikanayo kama Gassava Starch of Tanzania Corporation (CSTC), Christophe Gallean, amesema kiwanda hicho kitaweza kuzalisha tani moja kila siku za unga wa muhogo.Ameongeza kuwa ni furaha yao kuona kuwa wameanzisha rasmi kiwanda cha kwanza cha ubora wa hali ya juu na cha kisasa nchini Tanzania. Alisema kiwanda hicho kilianzishwa miaka saba iliyopita kwa lengo la kuuza unga wa muhogo wenye ubora wa hali ya juu ndani ya nje ya nchi.

    Aliongeza kuwa kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kusafirisha bidhaa zake katika masoko muhimu duniani yakiwamo ya Afrika ya Mashariki na Kusini, Mashariki ya Kati, Marekani na Ulaya.

    Amesisitiza kuwa mfumo wa Utendaji wa CSTC ni kukuza mazao yenye ubora wa hali ya juu katika mashamba makubwa yenye ufanisi na kusimamiwa na CSTC. CSTC ilianza kufanya kazi mwaka 2012, nchini humo ikiwa na wafanyakazi zaidi ya 400 ambao kati yao asilimia 97 ni Watanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako