• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanya biashara watakiwa kuuza bidhaa zao nje ya nchi

    (GMT+08:00) 2019-03-26 18:49:58
    Shirika la Viwango nchini Tanzania (TBS) limewataka wazalishaji wenye bidhaa zilizokidhi matakwa ya viwango na kukabidhiwa leseni za kutumia alama ya ubora, kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kupanua masoko yao ikiwa ni pamoja na kuuza bidhaa zao nje ya nchi. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TBS, Prof. Makenya Maboko amesema alama ya ubora ni muhimu sana katika biashara kwa kuwa inampa mzalishaji uhakika kuhusu ubora na usalama wa bidhaa yake, hivyo kumjengea imani kwa walaji.

    Ameongeza kuwa alama ya ubora pia humsaidia mzalishaji kupanua masoko ya bidhaa zake nje ya nchi na ni wazi kuwa hatua hiyo ni ya kujivunia sana kama mzalishaji na kama taifa kupanuka kwa masoko ya kikanda na kimataifa kutasaidia kuongeza fedha za kigeni na hatimaye kusaidia kukuza uchumi.

    Alifafanua kuwa hali hiyo itasaidia kufikiwa kwa azima ya taifa ya kujenga uchumi wa kati unaotegemea uzalishaji wa viwandani ifikapo mwaka 2025.

    Aliwataka wazalishaji waliopatiwa leseni hizo kuzingatia masharti yake na kuwa waadilifu katika uzalishaji wao, ili kuhakikisha wanaendelea kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango wakati wote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako