• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopian Airline kuendelea kushirikiana na Boeing

    (GMT+08:00) 2019-03-26 18:50:34

    Shirika la ndege la Ethiopian Airlines limesema kuwa bado lina imani na kampuni ya kutengeneza ndege ya Marekani Boeing licha ya ajali iliyohusisha ndege ya aina hiyo 737 Max, iliyotengenezwa na kampuni hiyo na kusababisha vifo vya watu 157.

    Mkuu wa shirika hilo Tewolde Gebremariam amesema Licha ya maafa , Boeing na Ethiopian Airlines wataendelea kuwa na uhusiano mwema siku zijazo "

    Aidha Tewolde pia amesema kuwa mfumo wa usalama wa ndege ulikuwa unanya kazi kabla ya mkasa. Muundo ulibainika kuwa ndio tatizo katika ajali nyingine ya ndege ya Boeing 737 Max. Tewolde amesema Boeng wamekuwa washirika wao kwa miaka mingi.Zaidi ya theluthi mbili ya safari za ndege za Ethiopia hufanywa na ndege zilizotengenezwa na Boeing.

    Ethiopian Airlines pia imeagiza ndege nyingine zaidi ya Boeing 25 Max 737 , baada ya kununua ndege tano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako