• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Muungano wa Kimataifa lasaini makubaliano na Umoja wa Mataifa ili kuimarisha ulinzi wa watoto wa Yemen

    (GMT+08:00) 2019-03-26 19:22:00

    Shirika la habari la Saudi Arabia limesema, jeshi la muungano wa kimataifa linaloongozwa na nchi hiyo limesaini makubaliano na Umoja wa Mataifa, ili kuimarisha ulinzi kwa watoto wa Yemen wanaoathiriwa na mapigano.

    Kamanda wa jeshi hilo Bw. Fahad Bin Turki Bin Abdulaziz na mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya watoto na masuala ya mapigano ya kivita Bibi Virginia Gamba wamesaini makubaliano hayo, ili kuchukua hatua zaidi kuwalinda watoto nchini Yemen.

    Bi Gamba amesema, katika miezi miwili ijayo, jeshi hilo na Umoja wa Mataifa utafuata lengo la kuwalinda watoto na kuzindua kazi za utoaji wa mafunzo ya pamoja na kueneza ujuzi husika wa ulinzi wa watoto. Amesema mwezi ujao, Umoja huo pia utafanya kampeni ya kimataifa jijini New York yenye kaulimbiu ya mgogoro unaowakabili watoto nchini Yemen.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako