Kwa mujibu wa kamisheni ya Ulaya, Nike iliingia mikataba isiyo halali kisheria kwa vifaa kwa klabu za FC Barcelona, Manchester United, Juventus, Inter Milan na AS Roma pamoja na timu za taifa wakiwemo mabingwa wa soka duniani Ufaransa.
Kiongozi wa kamisheni hiyo Margrethe Vestager amebainisha kuwa, mashabiki wa soka hupenda kununua vifaa mbalimbali vilivyowekwa nembo za klabu zao ikiwemo skafu, jezi, Nike ilizuia aina hiyo ya bidhaa kwenye nchi nyingine na kusababisha mashabiki kutokuwa na uwanja mpana wa kuchagua ama kununua kwa bei kubwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |