• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Spika wa bunge la umma la China Bw. Li Zhanshu afanya mazungumzo na mwenzake wa Burkina Faso

    (GMT+08:00) 2019-03-27 09:32:00

    Spika wa bunge la umma la China Bw. Li Zhanshu jana hapa Beijing alifanya mazungumzo na mwenzake wa Burkina Faso Bw. Alassane Bala Sakande.

    Bw. Li ameipongeza Burkina Faso kwa kufanya uamuzi wa kisiasa wa kurudisha uhusiano wa kidiplomasia na China, na kushikilia msimamo wa kuwepo kwa China moja. Bw. Li amesema mafanikio makubwa ya ushirikiano yaliyopatikana tangu China na Burkina Faso zirudishe uhusiano wa kidiplomasia, yameonesha mustakabali mzuri wa ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili, pia yameonesha kuwa uamuzi huo unaambatana na maslahi ya kimsingi na ya muda mrefu ya Burkina Faso na wananchi wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako