• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bibi Peng Liyuan ahudhuria mkutano maalumu wa elimu kwa watoto wa kike na wanawake wa UNESCO

    (GMT+08:00) 2019-03-27 09:54:41

    Mke wa rais Xi Jinping wa China ambaye ni mjumbe maalumu wa kuhimiza elimu kwa watoto wa kike na wanawake wa UNESCO Bibi Peng Liyuan, jana huko Paris alihudhuria mkutano maalumu wa elimu kwa watoto wa kike na wanawake wa UNESCO.

    Bibi Peng Liyuan alitoa hotuba akisifu juhudi za UNESCO na washindi wa tuzo ya elimu kwa watoto wa kike na wanawake katika kuhimiza elimu hiyo. Amesisitiza kuwa kuhimiza elimu kwa watoto wa kike na wanawake ni jambo la maana linalostahili kuungwa mkono. Ujuzi na ustadi ni nguvu ya kubadilisha maisha ya wanawake, na kama wakipata elimu yenye usawa na ubora, kila mwanamke atakuwa na fursa ya kujitokeza maishani. Amesema China itaendelea kuunga mkono UNESCO kuendesha tuzo hiyo, na kutumia ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kuwa fursa na jukwaa la ushirikiano na maingiliano ya kimataifa kuhusu elimu, ili kuwasaidia watoto na wanawake wengi zaidi kupata mustakabali mzuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako