• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na viongozi wanaohudhuria ufungwaji wa baraza la usimamizi wa dunia kati ya China na Ufaransa

    (GMT+08:00) 2019-03-27 09:55:03

    Rais Xi Jinping wa China jana huko Paris amekutana na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya Bw. Jean Juncker ambao wamehudhuria ufungwaji wa baraza la usimamizi wa dunia kati ya China na Ufaransa.

    Rais Xi Jinping amesema China na Ulaya zinapaswa kushirikiana katika pande tatu, kwanza kulinda kwa pamoja hali ya nchi nyingi, pili, kuhimiza ustawi na maendeleo ya bara la Asia na Ulaya, tatu kuongeza hali ya kuaminiana ya kimkakati kati ya pande mbili.

    Rais Macron amesema, Ufaransa na Umoja wa Ulaya zinapenda kuimarisha hali ya kuaminiana na China, kuchukua kwa pamoja wajibu wa kuhimiza amani, usalama na maendeleo ya dunia.

    Bibi Merkel amesema, Ujerumani inatilia maanani umuhimu wa China katika mambo ya kimataifa, inapenda kushirikiana na China kuhimiza utaratibu wa kimataifa wenye ncha nyingi.

    Bw. Juncker amesema, Umoja wa Ulaya unapenda kuharakisha ushirikiano na China, ili kukabiliana na changamoto za dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako