• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Botswana aahidi kupunguza umasikini uliokithiri

    (GMT+08:00) 2019-03-27 16:05:24

    Rais Mokgweetsi Masisi wa Botswana amesema kupunguza umasikini uliokithiri ni kipaumbele cha serikali yake, na anajitahidi kuvutia wawekezaji wa kigeni kuwekeza nchini humo ili kutoa fursa za ajira.

    Rais Masisi amesema hayo alipozungumza na wajumbe wa chama tawala nchini humo (BDP) mjini Francistown, siku chache kabla ya kufanyika uchaguzi wa ndani wa chama. Amesema analenga kuimarisha hali ya maisha ya kila mwananchi nchini humo, na kuongeza kuwa ni muhimu kuwa na uhusiano wa pande nyingi na mashirika yasiyo ya kiserikali na kampuni binafsi ili kupambana na umasikini.

    Idadi ya watu wanaoishi chini ya mstari wa umasikini nchini Botswana imepungua kutoka asilimia 30.6 mwaka 2002/2003 hadi asilimia 16.3 mwaka 2015/2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako