• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ongezeko la mazao ya nyuki Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-03-27 19:09:10

    Uzalishaji wa mazao ya nyuki katika mashamba ya serikali ya ufugaji nyuki yaliyopo mikoa ya Dodoma na Singida unatarajia kuongezeka hadi kufikia zaidi ya tani tisa za asali ikilinganishwa na miaka iliyopita.

    Ni shughuli ya uvunaji wa mazao ya nyuki katika mashamba ya serikali yaliyopo wilayani Manyoni mkoani Singida, na Kondoa mkoani Dodoma, ambapo Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Kati, Methew Kiondo, alisema miaka iliyopita mavuno ya mazao ya nyuki yalikuwa ndoo 10 hadi 20, lakini mwaka huu uzalishaji umeongezeka maradufu.

    Kiondo alisema ufanisi huo umetokana na mapinduzi yaliyofanywa katika sekta ya ufugaji nyuki kwenye mashamba hayo yaliyopo katika wilaya hizo, ambapo jitihada zaidi zimeimarishwa kwenye usimamizi wa karibu wa makundi ya nyuki.

    Uwapo wa mashamba hayo ya serikali unawanufaisha wananchi kwa kuwapatia ajira na elimu ya utengenezaji wa mizinga ya kisasa kwa ajili ya ufugaji wa nyuki.

    Abdala Ali Bali, mkazi wa Kijiji cha Mialo Dodoma, alisema miradi hiyo itawasaidia sana kupata maendeleo kwa mfano wananchi wameanza kutengeneza barabara, kijiji kupata asilimia ya fedha zake na kutunza mazingira.

    Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Wafugaji Nyuki Tanzania (TAPEDO), Rodia Issa, ambaye pia ni mnufaika wa shughuli za ufugaji na uzalishaji wa mazao ya nyuki wilayani Kondoa, alieleza changamoto ya upatikanaji wa vifungashio na gharama kubwa ya mitambo ya kuchakata mazao ya nyuki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako