• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bodi ya maziwa yatangaza kusitisha 'sheria dhalilishi'

    (GMT+08:00) 2019-03-27 19:10:07
    Bodi ya kusimamia Sekta ya Maziwa Nchini Kenya (KDB) imeitikia wito wa wadau katika sekta hiyo na kusimamisha utayarishaji wa sheria zilizolenga kudhibiti sekta ya maziwa nchini.

    Sheria hizo tisa zilisitishwa hata kabla ya kuwasilishwa bungeni kujadiliwa na kuidhinishwa kwa mujibu wa Sheria inayosimamia sheria ndogo zinazotungwa na mashirika ya serikali (Statutory Instruments Act) ya 2013.

    Kulingana na Sheria hiyo, sheria zote ndogo zinazotungwa na mashirika ya serikali sharti ziidhinishwe na wabunge.

    Mkurugenzi Mkuu wa KDB Margaret Kibogy alisema hatua hiyo ya kusitishwa kwa sheria hizo imechukuliwa ili kutoa nafasi kwa mashauriano na ushirikishwaji wa umma.

    Sheria hizo ambazo wadau, mashirika ya kijamii na viongozi wa kisiasa, wametaja kama dhalimu, zinapiga marufuku uuzaji wa maziwa yasiyotayarishwa kwa watu wa kawaida. Wakulima wanatakiwa kupeleka maziwa yao kwa kiwanda chenye mitambo ya jokovu (cooling facility). Wakulima ambayo watapatikana na hatia ya kukiuka amri hiyo wataadhibiwa kwa kutozwa faini ya kiasi kisichozidi Sh500,000 au kifungo kisichozidi miaka miwili gerezani au adhabu zote mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako