• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Njaa yaendelea kushuhudiwa Kenya huku mahindi yakioza

    (GMT+08:00) 2019-03-27 19:10:24
    Wakulima Kaskazini mwa Rift Valley nchini Kenya wanahesabu hasara baada ya mahindi yao kuanza kuoza kwa kukosa mahala pa kuyauza, huku Shirika la Msalaba Mwekundu (KRCS) likikubali kuwa watu kadhaa wamekufa kutokana na njaa.

    Katibu Mkuu wa KRCS Abbas amesema inashangaza kuona watu wamekufa kutokana na sababu tofauti ikiwa ni pamoja na njaa na ukame huku mahindi yakiendelea kuoza Rift Valley. Wakulima wa mahindi eneo la North Rift wanasema serikali imeacha kununua mahindi na sasa yameanza kuharibika. Kwa sasa bei ya mahindi imeshuka hadi Sh1,500 kwa gunia la kilo 90, huku wakulima wakilazimika kuyauza kwa bei hiyo ili wapate pesa za kununua pembejeo kabla ya msimu wa upanzi.

    NCPB inanunua gunia ya kilo 90 kwa Sh2,500 lakini wakulima wengi wamefungiwa nje kufuatia masharti makali.Bei hiyo imeshuka huku ile ya mbolea ikipanda hadi Sh3,500 baada ya Serikali kushindwa kuagiza fatalaiza ya bei nafuu ambayo ingeuzwa Sh1,500 kwa gunia la kilo 50.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako