• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mifugo yaleta hasara kwenye mashamba

    (GMT+08:00) 2019-03-27 19:10:40

    Makundi ya mifugo kutoka wilaya jirani za Simanjiro na Mwanga yamevamia mashamba ya wakulima katika kijiji cha Mikocheni kilichoko kata ya Arusha Chini, Moshi Vijijini na kuharibu mazao ya chakula.

    Ofisa wa serikali katika eneo hilo Emmanuel Mosha amesema kuwa makundi hayo yamelalamikiwa na wakulima kuharibu mazao yao.

    Hiyo mifugo ambayo ni makundi ya ng'ombe tayari imesababisha hasara kubwa kwa wakulima.

    Wamiliki wa mashamba wameiomba kukaa meza moja na serikali kutafuta suluhu ya kudumu ya suala hilo ili kuzuia kujitokeza kwa matukio ya uvunjifu wa amani.

    Suala hilo limekuwa likitafutiwa ufumbuzi na viongozi wa wilaya jirani pamoja na Wilaya ya Moshi lakini wakulima wanasema kuna haja wafugaji wakatozwa faini kubwa kwa kosa hilo ili kuwakatisha tamaa ya kuhama na mifugo na kulisha mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako