• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasisitiza tena kuwa "mpango wa kuwepo kwa nchi mbili" ni njia pekee ya kutatua mapambano kati ya Palestina na Israel

    (GMT+08:00) 2019-03-27 19:26:04

    Naibu balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao jana amesema "mpango wa kuwepo kwa nchi mbili" ni njia pekee ya kutatua mapambano kati ya Palestina na Israel, na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuharakisha mchakato wa kuhimiza kurejeshwa kwa mazungumzo, ili kutatua suala la Palestina.

    Balozi Wu amesema hayo alipohudhuria mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Mashariki ya Kati. Amesema hali ya sasa ya Ukanda wa Gaza inaleta wasiwasi mkubwa, na China inasisitiza tena kuwa pendekezo jipya lolote linapaswa kusaidia kutimiza mpango wa kuwepo kwa nchi mbili.

    Ameongeza kuwa pande zote husika zinatakiwa kutekeleza azimio namba 2334, kusimamisha shughuli zote za ujenzi wa makazi kwenye ardhi inayokaliwa, kusitisha vurugu dhidi ya raia, na kufikia utatuzi wa suala unaolingana maslahi ya pande zote kupitia mazungumzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako