• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China akutana na mkurugenzi wa Baraza la Asia la Boao

    (GMT+08:00) 2019-03-27 20:50:20

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo mkoani Hainan, kwa nyakati tofauti amekutana na mkurugenzi wa Baraza la Asia la Boao Bw. Ban Ki-moon, pamoja na mawaziri wakuu wa Laos, Sao Tome, na Principe.

    Wakati wa mazungumzo hayo Bw. Li amesisitiza kuwa China ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, bado inakabiliwa na njia ndefu katika kutimiza kwa pande zote mambo ya kisasa. Amesema China inatetea utaratibu wa pande nyingi, na kuheshimu utamaduni anuwai wa binadamu, pia inaunga mkono nchi mbalimbali zitafute njia ya kujiendeleza kwa kufuata hali yao.

    Naye Bw. Ban Ki-moon amesema, China, Bara la Asia na dunia kwa ujumla zitaunganishwa kwa ukaribu katika siku za baadaye, na baraza hilo linapenda kushirikiana na pande mbalimbali ili kuhimiza mafungamano ya kiuchumi barani Asia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako