• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Michuano ya kufuzu Olimpiki 2020 Japan. Twiga Stars uso kwa uso na Les Leopards

    (GMT+08:00) 2019-03-28 08:14:28
    Timu za taifa za wanawake za soka ya Tanzania (Twiga Stars) na ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC (Les Leopards) zitashuka katika dimba la taifa jijini Dar es Salaam Aprili 5 mechi ya kufuzu michuano ya Olimpiki mwaka 2020 itakayofanyika Japan.

    Wakizungumza na waandishi wa habari, mmoja wa wachezaji wa timu ya Twiga Stars Fatuma Mustapha amesema, wapo tayari kuwakilisha na kupeperusha vyema bendera ya Tanzania na kuwataka mashabiki kujazana kwa wingi kwani watawaonyesha burudani ya kutosha.

    Nao Les Leopards wanaendelea na kambi mjini Goma Kaskazini mwa Kivu wakijifua kwa michezo kadhaa ya kirafiki ikiwemo na timu ya taifa ya Rwanda. Jumla ya wachezaji 26 wameitwa kwenye kambi hiyo.

    Mchezo wa marudiano utapigwa April 9 jijini Kinshasa DRC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako