• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wabunge wa Uingereza wapiga kura kubadilisha tarehe ya Brexit kuwa Aprili 12 au Mei 22

    (GMT+08:00) 2019-03-28 08:41:09

    Wabunge wa Uingereza wamepitisha kwa kura nyingi uamuzi wa kubadilisha tarehe rasmi ya kisheria ya Brexit kuwa Aprili 12 au Mei 22, wakati waziri mkuu Bibi Theresa May anajitahidi kuwashawishi wabunge wa chama cha wahafidhina kuunga mkono makubaliano yake ya Brexit.

    Wabunge walipiga kura 441 za ndio na 105 za hapana kwenye baraza la makabwela, kuipitisha tarehe mpya ya Brexit kuwa sheria na kufuta mpango wa awali wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya Machi 29.

    Mkanganyiko kuhusu Brexit bado unaendelea nchini Uingereza kutokana na kuwa wabunge wa nchi hiyo wameshindwa kupata uungaji mkono wa kutosha kuhusu mpango mbadala wa makubaliano ya Bibi Theresa Mei.

    Aidha, wabunge pia wamepitisha maamuzi ya kukataa kujitoa Umoja wa Ulaya bila makubaliano, na kukataa ombi la kupiga tena kura za maoni juu ya Brexit.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako