• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia yawatahadharisha raia wake nchini Afrika Kusini baada ya kutokea mashambulizi mapya dhidi ya wageni

    (GMT+08:00) 2019-03-28 08:41:36

    Serikali ya Zambia imetahadharisha wananchi wake wanaoishi nchini Afrika Kusini kufuatia ripoti za kutokea kwa mashambulizi mapya dhidi ya wageni.

    Ripoti zinasema wageni wanaoishi nchini Afrika Kusini wameshambuliwa haswa katika mkoa wa Kwazulu Natal, na video za mashambulizi hayo zimewekwa kwenye mitandao ya kijamii.

    Balozi wa Zambia nchini Afrika Kusini Bw. Emmanuel Mwamba amesema mpaka sasa hakuna mzambia aliyeathiriwa na mashambulizi hayo, na pia amewataka raia wa Zambia wachukue tahadhari na kwamba ubalozi unafuatilia kwa karibu matukio hayo.

    Balozi huyo ametoa wito kwa wanasiasa wa Afrika Kusini kuwa makini na kauli zao kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Mei, kwa kuwa kauli yoyote dhidi ya wageni wanaoishi nchini humo, inaweza kuchochea chuki dhidi ya wageni, na kusababisha uharibifu wa mali na hata mauaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako