• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tuzo ya Jack Ma ya wajasiriamali kwenye mtandao yazinduliwa Kenya kuhimiza uhusiano kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2019-03-28 08:59:10

    Tuzo ya mjasiriamali kwenye mtandao inayoungwa mkono na mwasisi wa kampuni ya Alibaba Bw. Jack Ma, ilizinduliwa jana nchini Kenya ili kuhimiza ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Mkuu wa Kampuni ya Nailab, ambayo ni mdau wa tuzo hiyo barani Afrika na katika eneo la Afrika Mashariki Bw. Sam Gachiru, amewaambia wanahabari mjini Nairobi kuwa tuzo hiyo imeandaliwa kwa ajili ya waafrika wanaofanya biashara barani Afrika.

    Amesema tuzo hiyo ina lengo la kuhimiza ushirikiano kati ya China na Afrika, na inaonesha kuwa China ni mdau wa karibu wa Afrika na inapenda kutoa mchango katika kuwainua watu wanaoishi kwenye umaskini kupitia ujasiriamali.

    Maombi kwa ajili ya tuzo hiyo yamefunguliwa kwa pamoja nchini Nigeria, Misri, Kenya na Afrika kusini, watu 10 wataingia fainali kugombea dola milioni moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako