• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shehena ya kwanza ya msaada wa UNHCR yafika Msumbiji

    (GMT+08:00) 2019-03-28 09:19:10

    Ndege ya Shirika la kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR yenye msaada kwa watu walioathiriwa na kimbunga cha Idai imefika Maputo, Msumbuji.

    Hii ni shehena ya kwanza kati ya tatu kutolewa na UNHCR kwa ajili ya watu waliokumbwa na kimbunga hicho nchini Msumbiji, Zimbabwe na Malawi.

    Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema, msaada huo ambao ni pamoja na mahema, mablanketi, vyandarua, na taa za kutumia nishati ya jua utafikishwa kwa watu elfu 30 nchini Msumbiji, Malawi na Zimbabwe, huku timu za dharura za UNHCR zikitumwa katika nchi hizo tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako