• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaihimiza jumuiya ya kimataifa kuunga mkono mchakato wa kisiasa nchini Syria

    (GMT+08:00) 2019-03-28 09:19:37

    Naibu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao ameitaka jumuiya ya kimataifa iendelee kusukuma mbele mchakato wa kisiasa nchini Syria.

    Balozi Wu amesema mapambano yaliyodumu kwa miaka mingi yameleta maumivu makubwa kwa watu wa nchi hiyo, na wanatamani amani irudi mapema, ili kurudisha maisha ya utulivu.

    Amesema Umoja wa Mataifa unatakiwa kuimarisha ushirikiano na serikali ya Syria, ili kuhimiza kujenga mapema kamati ya katiba inayowakilisha na kupokelewa na pande zote.

    Aidha, Bw. Wu amehimiza jumuiya ya kimataifa kuongeza ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugaidi nchini Syria, na kutumia vigezo vya pamoja katika kupambana na makundi yote ya kigaidi yaliyoorodheshwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ili kuyazuia yasirudi nchini humo.

    Habari nyingine zinasema vikosi vya anga vya Syria vilizuia makombora kadhaa yaliyorushwa na Israel katika jimbo la Aleppo kaskazini mwa Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako