• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Uganda azitaka nchi za Afrika Mashariki zinunue bidhaa za kanda hiyo

    (GMT+08:00) 2019-03-28 09:27:57

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda jana amezitaka nchi za Afrika Mashariki zinunue bidhaa zilizotengenezwa katika kanda hiyo, ili kupunguza uagizaji wa bidhaa ambazo zinaweza kutengenezwa huko.

    Rais Museveni anayefanya ziara ya siku mbili nchini Kenya amesema, nchi za Afrika Mashariki zinalazimika kutoa mamilioni ya dola kwenye uagizaji wa bidhaa, kwa sababu viwanda vikubwa kwenye kanda hiyo vimefungwa.

    Rais Museveni ameitaka Kenya ifufue mapema Kiwanda cha karatasi cha Webuye, ambacho kilikuwa muhimu katika kutoa bidhaa za karatasi kwa Afrika Mashariki. Ameongeza kuwa Uganda inaagiza karatasi zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 130 kutoka Finland, lakini Kenya ina kiwanda cha kutengeneza karatasi kilicholala.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako