• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ashuhudia mara kadhaa za kwanza katika ziara yake barani Ulaya

    (GMT+08:00) 2019-03-28 10:25:08

    Kuanzia tarehe 21 hadi 26, rais Xi Jinping wa China alifanya ziara nchini Italia, Monaco na Ufaransa, na kushuhudia mara kadhaa za kwanza kwenye mambo ya kidiplomasia kati ya China na Ulaya.

    Italia imekuwa nchi ya kwanza ya kundi na G7 inayojiunga na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Rais Xi na waziri mkuu wa Italia Bw. Giuseppe Conte walishuhudia kwa pamoja kusainiwa kwa waraka wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kuhusu ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Rais Xi alifanya ziara nchini Monaco ambayo ni ziara ya kwanza kwa rais wa China nchini humo. Monaco ni nchi ndogo yenye eneo la kilomita mbili za mraba, na ziara hiyo inaonesha kuwa China inafuata mawazo ya kuzitendea nchi zote kwa usawa.

    Rais Xi pia alihudhuria kongamano la kwanza la usimamizi wa dunia kati ya China na Ufaransa, na kutoa hotuba ya "kutoa busara na mchango kwa ajili ya ujenzi wa dunia yenye uzuri zaidi".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako