• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini yamteua mkurugenzi wa Mamlaka ya Kodi nchini humo

    (GMT+08:00) 2019-03-28 15:57:46

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amemteua Edward Kieswetter kuongoza Mamlaka ya Kodi ya nchi hiyo (SARS).

    Rais Ramaphosa amesema, wana uhakika kuwa Bw. Kieswetter ana uzoefu, maadili na ujuzi unaotakiwa kufanya mageuzi kwa mamlaka hiyo kwa kurejesha ukusanyaji kodi, kuelekeza uvumbuzi katika operesheni mbalimbali, kuandaa viongozi wajao katika mamlaka hiyo, na kurejesha uaminifu na ufanisi wa mamlaka hiyo.

    Wizara ya Fedha ya nchi hiyo imesema, uteuzi huo utaanza rasmi Mei Mosi mwaka huu, na Bw. Kieswetter atashikilia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka mitano. Uteuzi huo unatarajiwa kuimarisha mamlaka ya Kodi nchini Afrika Kusini katika wakati ambao ukusanyaji wa kodi na haki ya kodi ni muhimu kwa kufufua uchumi wa nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako