• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito wa kuendelea kuhimiza mchakato wa utatuzi wa suala la Syria kwa njia ya kisiasa

    (GMT+08:00) 2019-03-28 17:03:06

    Naibu balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao ametoa wito wa kuendelea kuhimiza mchakato wa utatuzi wa suala la Syria kwa njia ya kisiasa.

    Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mchakato wa kisiasa wa suala la Syria uliofanyika jana, balozi Wu amesema Umoja wa Mataifa unapaswa kuimarisha uratibu na serikali ya Syria na kuhimiza kuunda kamati ya katiba ya Syria inayokubaliwa na pande zote husika haraka iwezekanavyo. Pia kuzingatia kwa uwiano ufuatiliaji unaofaa kutoka serikali ya Syria na pande nyingine husika, ili kuanzisha mchakato endelevu wa kisiasa wa suala la Syria wenye ufanisi.

    Ameongeza kuwa jumuiya ya kimataifa inapaswa kuongeza kutoa msaada kulingana na mahitaji ya kibinadamu ya Syria, na kuunga mkono serikali na wananchi wa Syria katika kujenga upya maisha yao. Amesema China inaunga mkono kutatua suala la Syria kwa njia ya kisiasa, na inapenda kuimarisha mawasiliano na uratibu na Umoja wa Mataifa ili kufanya juhudi za kiujenzi juu ya suala hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako