• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China akutana na mawaziri wakuu wa Korea Kusini na Luxemburg

    (GMT+08:00) 2019-03-28 19:32:30

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang kwa nyakati tofauti amekutana na mawaziri wakuu wa Korea Kusini Bw. Lee Nak-yon na Luxemburg Bw. Xavier Bettel ambao walihudhuria Baraza la Asia la Boao lililofanyika mkoani Hainan.

    Alipokutana na waziri mkuu wa Korea Kusini Bw. Li, amesema China ina nia ya kufanya juhudi na Korea Kusini ili kuimarisha uaminifu, mawasiliano na ushirikiano, na kukuza maendeleo mapya katika uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Pia China ina nia ya kuharakisha mchakato wa mazungumzo ya eneo la biashara huria la China-Japan-Korea Kusini (FTA), kuhimiza mafungamano ya kiuchumi kwenye kanda hiyo, na kulinda kwa pamoja ustawi na utulivu wa kikanda.

    Waziri mkuu wa Korea Kusini Lee Nak-yon amesema nchi yake ina nia ya kujiunga na pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", kuimarisha ushirikiano na China katika nyanja mbalimbali, na kulinda pamoja utaratibu wa pande nyingi na biashara huria.

    Alipozungumza na waziri mkuu wa Luxemburg, Bw. Li amesema China ina nia ya kufungua mlango zaidi na upande wa Luxemburg, kuimarisha uhusiano wa kisiasa na kiuchumi, na kuimarisha ushirikiano wa kisayansi, hasa ushirikiano wa kifedha, ili kufikia maendeleo ya kawaida.

    Kwa upande wake, waziri mkuu wa Luxemburg Bw. Bettel amesema nchi yake inaunga mkono nchi za Ulaya na China kuendeleza uhusiano wa ushirikiano na kimkakati wa pande zote, kujenga pamoja pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na kuimarisha ushirikiano na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako