• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi kadhaa zapinga uamuzi wa Marekani wa kuikubali Israel kudhibiti mamlaka ya Milima ya Golan

    (GMT+08:00) 2019-03-28 19:48:48

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana lilikutana na kujadili suala la Milima ya Golan, ambapo nchi wajumbe wote wa Baraza hilo isipokuwa Marekani wamepinga na kulaani uamuzi wa rais Donald Trump wa Marekani kuhusu kuikubali rasmi Israel kudhibiti mamlaka ya Milima hiyo.

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya siasa na ulinzi wa amani Bi. Rosemary DiCarlo alitoa ripoti kwenye mkutano huo na kusema, Umoja wa Mataifa umeweka bayana msimamo wake juu ya suala la mamlaka ya Milima ya Golan, na amepinga mtu yeyote kutumia kisingizio cha hali ya maendeleo ya hivi sasa kwa ajili ya kuharibu hali ya Milima ya Golan na maeneo mengine husika.

    Naibu balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema Milima ya Golan inachukuliwa na jumuiya ya kimataifa kuwa ni ardhi inayokaliwa. China inapinga kubadilisha hali halisi kupitia kitendo cha upande mmoja, pia haitaki hali ya kanda hiyo iendelee kuwa mbaya zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako