• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Asilimia 94 ya watanzania wafikiwa na huduma ya mawasiliano,asema Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi,Mhandisi Isaack Kamwelwe

    (GMT+08:00) 2019-03-28 19:52:05

    Takriban asilimia 94 ya ya wananchi wa Tanzania wamefikiwa na huduma ya mawasiliano huku minara 530 ikisimikwa katika maeneo mbalimbali nchini humo.

    Hayo yalibainishwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaack Kamwelwe, wakati alipokuwa akifungua Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo sekta ya mawasiliano.

    Mhandisi Kamwelwe alisema mbali na hilo sekta hiyo imewezesha taasisi mbalimbali kutumia mifumo ya kielektroniki kwa ajili ya kukusanya mapato na kutoa huduma ndani ya serikali na wananchi.

    Pia serikali kupitia sekta ya mawasiliano imekamilisha uandaaji wa mkakati wa taifa wa usalama wa mtandao.

    Alisema katika kuhakikisha sekta ya mawasiliano inakua, serikali inashirikiana na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na shughuli za mawasiliano zikiwamo sekta binafsi na wadau wengine katika kuendeleza kukuza sekta hiyo.

    Alisema hadi sasa kuna laini zaidi ya milioni 45 za simu za mkononi na watumiaji wa intaneti wapatao milioni 23.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako