Mwenyekiti wa kamati ya kilimo Bungeni,Emmanuel Wangwe jana alisema serikali haifai kuendelea kuagiza kugiza bidhaa hiyo ilhali kiwango cha maziwa kinachozalishwa nchini kinatosehleza mahitaji ya soko.
Aidha Wangwe,amabye pia ni mbunge wa Navakholo alisema Kenya inazalisha kilo 5.7 bilioni za maziwa kila mwaka ilhali hitaji la kitaifa ni kilo 5.2 bilioni pekee.
Aliongeza kuwa mwenendo huo wa serikali wa kuendelea kuagiza maziwa kutoka nje unawaumiza wakulima na unapasa kusitishwa mara moja.
Alisema uagizaji huo umechangia kupungua kwa bei ambayo wafugaji huuza maziwa yao kwa kampuni za kutayarisha maziwa kutoka Sh42 hadi Sh28 kwa lita moja.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |