• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya utoaji wa misaada ya China yaendelea na kazi kwa utaratibu nchini Msumbiji

    (GMT+08:00) 2019-03-28 19:59:44

    Timu ya uokoaji ya China iliyokwenda nchini Msumbiji kusaidia waathirika wa kimbunga Idai kilichoikumba nchi hiyo imerejea kwa usalama kwenye kambi yake baada ya kumaliza operesheni ya uokoaji.

    Timu hiyo ilitoa huduma za matibabu kwa watu mia tano walioathirika na maafa hayo, na kutoa elimu ya kinga na tiba ya magonjwa ya kuambukiza kwa wakazi kwenye kituo cha watu walioathirika na maafa kilichoko kilomita 10 kutoka kambi ya timu hiyo.

    Timu hiyo ya China yenye watu 65 wakiwa na vifaa na tani 20 za vifaa vya uokoaji, upashanaji wa habari na matibabu, ilianza kutoa misaada nchini Msumbiji jumatatu wiki hii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako