• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Safari ya wanariadha mbio za nyika za dunia yaiva

    (GMT+08:00) 2019-03-29 08:16:52
    Safari ya kikosi cha wanariadha wa timu ya taifa ya riadha ya Tanzania kushiriki mbio za dunia za nyika imeiva. Timu hiyo imeagwa na kuondoka jana usiku jijini Dar es Salaam tayari kwenda mjini Aarhs Denmark kwenye mashindano hayo yatakayofanyika Machi 30 mwaka huu.

    Katibu mkuu wa shirikisho la raidha Tanzania (RT) Wilhelm Gidabuday ameeleza kuwa jumla ya wanariadha 28 walikuwa kambini kujiandaa kwa mashindano hayo, na wako tayari na wana ari kubwa ya kurejea na medali.

    Msafara wa timu hiyo unaundwa na watu 20, wachezaji 16 na viongozi 4.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako