• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Samuel Etoo agusa nyoyo za watoto

    (GMT+08:00) 2019-03-29 08:17:09
    Nyota wa soka wa Cameroon Samuel Eto'o amegusa nyoyo za watu hususani watoto baada ya kutembelea kambi ya wakimbizi iliyopo katika mji wa Bertoua nchini Cameroon.

    Nyota huyo alitumia fursa hiyo kucheza na watoto wakimbizi kusakata kabumbu, huku yeye akicheza nafasi ya golikipa.

    Kuhusiana na ziara hiyo, Eto'o amesema, anataka watoto wa wakimbizi kutoka Afrika ya kati wajisikie vizuri huku lengo lake kubwa ni kuona watoto hao wanaambatana na wazazi wao kurejea makwao katika hali ya usalama.

    Eto'o alishindwa kujizuia kutokwa machozi baada ya kushuhudia vipaji mbalimbali vya michezo walivyonavyo watoto hao na kuahidi kuwasaidia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako