• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa nishati wa Afrika kusini atetea makubaliano ya mafuta na Sudan kusini

    (GMT+08:00) 2019-03-29 08:29:50

    Waziri wa nishati wa Afrika Kusini Bw. Jeff Radebe amepinga ukosoaji dhidi ya makubaliano ya mafuta na Sudan kusini, akisema Afrika kusini inatakiwa kufanya kilicho sahihi ili kufikia mahitaji yake ya nishati.

    Waziri huyo amesema hayo alipojibu ripoti iliyochapishwa na gazeti la Sunday Times wiki iliyopita, iliyofichua makubaliano ya mafuta yenye thamani ya dola bilioni moja za kimarekani na Sudan Kusini, na kudai kuwa timu ya Bw. Radebe ilitumia ovyo fedha nyingi kwa ajili ya kununua mafuta kutoka Sudan Kusini.

    Waziri huyo amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha upatikanaji wa mafuta kwa Afrika Kusini, ili kukidhi mahitaji ya ndani na kutafuta njia za kutuliza bei ya mafuta katika kipindi kirefu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako