• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Uingereza leo linapigia kura tena makubaliano ya Brexit

    (GMT+08:00) 2019-03-29 08:59:33

    Baraza la chini la bunge la Uingereza leo linapiga kura kuhusu makubaliano mengine ya kujitoa Umoja wa Ulaya, ili kuondoa mkwamo wa sasa wa Brexit.

    Uamuzi huo umefikiwa baada ya mjadala uliofanyika jana bungeni, wakati makubaliano mengine kama hayo yamekataliwa bungeni mara mbili tangu mwezi januari.

    Spika wa baraza la makabwela la bunge la Uingereza Bw. John Becrow jana alisema bungeni kuwa mswada huo utakaopigiwa kura ni "mpya na una mabadiliko makubwa" na umeidhinishwa kupigiwa kura leo. Mswada huo utapigiwa kura wakati jumuiya ya wafanyabiashara inaendelea kukasirishwa na mkwamo wa Brexit.

    Hata hivyo aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Bw. Boris Johnson amesema makubaliano ya Bibi May, yamekufa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako