• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa mwito wa kupambana na vitendo vya kugharamia ugaidi

    (GMT+08:00) 2019-03-29 08:59:56

    Mjumbe wa China katika Umoja wa mataifa Bw. Ma Zhaoxu ameitaka jumuiya ya kimataifa iimarishe ushirikiano na kujenga uwezo kati ya nchi wanachama kwenye mapambano dhidi ya vitendo vya kufadhili ugaidi.

    Akiongea kwenye mjadala wa wazi ulioitishwa na Ufaransa, ambayo ni mwenyekiti wa zamu ya mwezi Machi wa baraza la usalama, Balozi Ma amesema kupambana na vitendo vya kufadhili ugaidi ni kazi yenye utatanishi, na nchi nyingi zinazoendelea zinakabiliana na changamoto ya kukosa uwezo wa usimamizi wa fedha na raslimali.

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia mapambano dhidi ya ugaidi Bw. Vladmir Voronkov pia amesema kwenye mkutano huo kuwa mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea katika siku za hivi karibuni yanaonesha kuwa fedha bado zinaendelea kuwafikia magaidi kutoka kwenye vyanzo haramu na halali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako