• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • StarTimes kutoa kipaumbele kwa maudhui ya kienyeji ili kuwavutia watazamaji wa Kenya

    (GMT+08:00) 2019-03-29 09:08:05

    Shirika la televisheni ya kulipia la StarTimes China limesema linapanga kutoa kipaumbele kwa maudhui ya kienyeji katika utengenezaji na utangazaji wa vipindi vya televisheni, ili kuongeza watazamaji wake wa Kenya.

    Mkuu wa tawi la StarTimes nchini Kenya Bw. Andy Wang amesema, shirika hilo litaanzisha kituo katika eneo la Karen, kitongoji cha Nairobi, ili kutengeneza vipindi vinavyowavutia watazamaji wenyeji.

    Bw. Wang amesema watafuatilia utamaduni mkubwa wa kiafrika na kutoa vipindi vipya vya burudani na elimu. Takwimu zinaonesha kuwa StarTimes inatoa huduma ya TV kwa karibu watu milioni 20 wa nchi 30 barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako