• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yashirikiana na UNESCO kuimarisha usimamizi wa Internet

    (GMT+08:00) 2019-03-29 09:08:25

    Sudan Kusini imeanzisha ushirikiano na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO, ili kuratibu sera na sheria husika za usimamizi wa Internet.

    Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya upashanaji habari ya Sudan Kusini Bw. Ladu Kenyi, amesema sera madhubuti zinapaswa kufuatwa ili kuimarisha usimamizi wa Internet kutokana na matishio ikiwemo uhalifu wa mtandaoni.

    Bw. Kenyi amesema serikali ya nchi hiyo inashirikiana na wadau wa kimaendeleo kwa ajili ya kuimarisha usalama wa miundombinu na data za kidigitali, na usalama wa mtandao ni muhimu zaidi katika kuhimiza maendeleo, amani na usalama wa taifa hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako