• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikosi cha uokoaji cha China chatoa msaada kwa watoto nchini Msumbiji

    (GMT+08:00) 2019-03-29 10:05:44

    Kikosi cha uokoaji cha China kimetoa msaada wa chakula na maji ya kunywa kwa mamia ya watoto walioko katika kituo cha yatima na shule katikati ya Msumbiji.

    Mkurugenzi wa kituo hicho cha eneo la Dondo katika jimbo la Sofala, Farruque Ribeiro amesema, kutokana na athari za kimbunga cha Idai, idadi ya watoto waliopokelewa na kituo hicho imeongezeka kutoka 330 hadi 480.

    Habari zinasema madaktari wa kikosi hicho pia wametoa matibabu kwa watoto wanaosumbuliwa na kuharisha na magonjwa mengine.

    Habari nyingine zinasema serikali ya Zimbabwe inahitaji dola za kimarekani milioni 83 kwa ajili ya ukarabati wa barabara na madaraja yaliyoharibiwa na kimbunga hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako