• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda kujenga vituo vidogo vya umeme kuhakikisha upatikanaji wa nishati hiyo

    (GMT+08:00) 2019-03-29 17:01:32

    Rwanda inatarajia kujenga vituo vidogo vya umeme kwa lengo la kuboresha sekta ya nishati nchini humo ili kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika.

    Waziri wa miundombinu nchini Rwanda Bw. Claver Gatete amesema hayo katika uzinduzi wa vituo vidogo vya umeme vya Nzove na Gahanga vilivyoko wilaya ya Bugesera, mkoa wa Mashariki nchini humo. Amesema, lengo la kufanya hivyo ni kuongeza idadi ya vituo vya nishati kutoka 27 vya sasa hadi kufikia 45 itakapofika mwaka 2024, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kuhakikisha umeme wa uhakika na wa kutosha kwa wananchi wake.

    Rwanda imeweka lengo la kutimiza upatikanaji wa umeme kwa wote itakapofika mwaka 2024, ambalo linatazamiwa kufikiwa kwa kupitia matumizi ya umeme wa maji na wa jua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako