• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zambia ataka hatua zaidi zichukuliwe kupunguza vifo vya wamama wajawazito

    (GMT+08:00) 2019-03-29 18:45:06

    Rais Edgar Lungu wa Zambia ametaka hatua zaidi za makini zichukuliwe kupunguza vifo vya wamama wajawazito nchini humo, licha ya kupungua kwa idadi ya wanawake wanaofariki wakati wa kujifungua.

    Rais Lungu amesema hayo wakati akipokea ripoti kuhusu utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa nchi hiyo utakaowapatia wananchi maisha bora zaidi, na kuielekeza ofisi ya Hazina kutoa fedha zinazotakiwa ili kuajiri wauguzi elfu 3 kukabiliana na tatizo hilo.

    Waziri wa afya wa nchi hiyo Chitalu Chilufya amesema, idadi ya wajawazito waliofariki wakati wakijifungua ilikuwa kati ya 35 na 40 kila wiki, lakini sasa idadi hiyo imepungua na kufikia kati ya nane na kumi. Amesema kuajiri wauguzi zaidi kutasaidia kupunguza zaidi idadi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako