• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Asilimia kubwa ya wakenya wanatamani kuhamia nchi nyingine kutokana na ugumu wa maisha

    (GMT+08:00) 2019-03-29 19:48:44
    Ripoti iliyotolewa na shirika linalotafiti masuala ya demokrasia, utawala na hali ya kiuchumi barani Afrika, Afrobarometer, inaonyesha kuwa asilimia 35 ya Wakenya wanatamani kuhamia mataifa ya kigeni kutokana na hali ngumu ya maisha humu nchini.

    Sababu nyingine zinazowasukuma Wakenya kuhamia mataifa ya kigeni ni masomo, kutalii na kutafuta nafasi za kibiashara..

    Mkurugenzi wa Afrobarometer Gyimah Boadi amesema asilimia 40 ya wanaume wanatamani kuhamia nchi za kigeni kwenda kusaka ajira ikilinganishwa na asilimia 33 ya wanawake.

    Aidha Ripoti hiyo inasema kuwa wakenya walio na hamu kubwa ya kuhamia nchi za kigeni kwenda kutafuta ajira ni vijana wa kati ya umri wa miaka 18 na 25.

    Ripoti hiyo inaendelea kusema kuwa zaidi ya nusu ya wakenya walio na elimu ya vyuoni wanatamani kuhamia ughaibuni.

    Jambo la kushangaza ni kwamba wengi wa Wakenya, asilimia 29, wanatamani kuhamia katika mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kama vile Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.

    Asilimia 27 wanatamani kuhamia mataifa ya Ulaya na Amerika (asilimia 22).

    Nchi ambazo raia wake wameridhika na hawatamani kuhamia nchi nyingine ni Madagascar, Tanzania na Mali mtawalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako