• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania haina wataalamu wa kusanifu madini,asema mwenyekiti wa TAMIDA

    (GMT+08:00) 2019-03-29 19:50:11

    Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara, Wanunuzi na Wauzaji wa Madini nchini (Tamida), Sammy Mollel, amesema Tanzania haina wataalamu wa kutosha wa kusanifu madini.

    Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mollel aliiomba serikali kuondoa urasimu katika utoaji wa vibali vya ajira pale wanapotaka kuleta wataalamu wa kigeni wa kusanifu madini.

    Alisema hivi sasa taratibu za kuomba vibali vya kuajiri wataalamu wa kigeni zinachukuwa mpaka miaka miwili kuweza kupata vibali.

    Aliongeza nchi inahitaji wataalamu wa hali ya juu katika ukataji, ung'arishaji na usanifu wa madini kutoka nchi zenye wabobezi hususani Sri-Lanka ili wasaidie kuleta teknolojia na kuacha ujuzi kwa Watanzania.

    Alisema suala la utaalamu wa kukata, kung'arisha na kusanifu madini ya vito halihitaji kuwa na shahada bali ni suala linalohitaji kipaji cha mtu mwenyewe katika kazi hiyo.

    Alitaja madini kama rubi na sapphire kuwa yanahitaji utaalamu wa hali ya juu na mashine za kipekee hasa katika uchomaji, ambapo alieleza kwa nchini Tanzania utaalamu wake haupo.

    Alisema hivi sasa nchi nzima ina mashine za kukata na kusanifu madini zisiozidi 300 ambazo kwa wastani zinauwezo wa kusanifu madini yasiozidi kilo moja kwa siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako