• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yatafuta uwekezaji baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kumalizika

    (GMT+08:00) 2019-03-29 19:50:10

    Sudan Kusini imefanya mkutano wa uwekezaji, ukiwa ni wa kwanza kufanyika baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, iliyodumu kwa miaka mitano.

    Mratibu wa mkutano huo Bw. Akol Nyok amesema, mkutano huo unaoitwa "Kufanya Biashara nchini Sudan Kusini" unalenga kuunganisha mashirika ya kimataifa, watu binafsi na mashirika binafsi na fursa za uwekezaji za nchi hiyo.

    Mkutano huo wa siku moja umewezesha maofisa wa serikali na wawekezaji wa ndani na nje kushiriki katika maonesho, vikao vya mawasiliano na majadiliano ya vikundi mbalimbali.

    Bw. Nyok pia amesema, kuna haja ya kuwasilisha habari kati ya watu wanaofanya biashara nchini humo na watu kutoka nje, huku akiongeza kuwa mkutano huo unaweza kuwa chombo cha kutoa habari halisi kwa watu wanaofanya biashara katika nchi hiyo yenye historia fupi zaidi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako