• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania haikusudii kunyanganya wala kutaifisha uwekezaji wa nje

    (GMT+08:00) 2019-03-30 17:25:13

    Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amesema Tanzania haikusudii kunyanganya wala kutaifisha uwekezaji wa nje.

    Kulingana na taarifa iliyotolewa na kitengo cha habari na mawasiliano cha wizara hiyo, Profesa Kabudi ametoa uhakikisho huo wakati wa mazungumzo yake na Lynda Chalker, mwanzilishi na rais wa Africa Matters Limited. Africa Matters Limited inafanya kazi na mashirika mbalimbali ya kimataifa, makampuni madogo na ya kati, serikali, washirika wenyeji na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhakikisha kwamba uwekezaji wa sekta binafsi unakuwa na jukumu muhimu katika kukuza mendeleo ya Afrika. Wakati wa mazungumzo, Kabudi amesema nchi hiyo hivi sasa inachunguza upya sheria zake za madini na sera na haikusudii kunyanganya au kutaifisha uwekezaji wa nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako