• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU yaitaka Afrika kuimarisha uwepo wake duniani ili kuongeza kasi ya mageuzi ya kidijitali

    (GMT+08:00) 2019-03-30 17:26:04

    Afrika imetakiwa kuimarisha sauti na uwepo wake kwenye mazungumzo ya dunia juu ya masuala yanayohusiana na data, usalama wa kimtandao na akili bandia.

    Wito huo umetolewa na nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika kufuatia kuzinduliwa kwa majadiliano mfululizo juu ya ushirikiano wa kidijitali na jopo la ngazi ya juu la Umoja wa Mataifa kuhusu Ushirikiano wa Kidijitali siku ya Alhamis.

    Umoja huo umesema teknolojia ya simu za mkononi imesaidia Afrika kuchupa na kuingia kwenye zama za kidijitali hasa katika muongo uliopita, ukisisitiza kuwa mageuzi ya kidijitali yamekuwa ndio kauli mbiu ya mikutano miongoni mwa viongozi wa Afrika chini ya mwavuli wa Umoja wa Afrika.

    Pia umesisitiza kuwa nchi za Afrika zinasonga mbele kwa utulivu, zikitumia kwa ufanisi teknolojia ya kidijitali kwenye elimu, kilimo, maendeleo ya uchumi na maeneo mengine husika, na kutaka Afrika ijiimarishe zaidi katika uwepo na uwekezaji kuelekea mageuzi ya kidijitali barani humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako