• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM kutoa ombi jipya la kusaidia wahanga wa kimbunga Idai

    (GMT+08:00) 2019-03-30 17:26:33

    Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema katika siku zinazofuata umoja huo unatarajiwa kutoa ombi jipya la kusaidia wahanga wa kimbunga Idai kusini mwa Afrika.

    Amefafanua kuwa kuhakikisha usalama wa chakula ni jambo litakalopewa kipaumbele, kwani mavuno ya mahindi, ambayo yataanza Mei, yatakuwa asilimia 60 ya uzalishaji wa wastani, ikiwa ni hatari zaidi ya kuzorota kwa usalama wa chakula. Naye naibu mratibu wa mambo ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Msumbiji Sebastian Rhodes Stampa amesema hali inatisha.

    Kulingana na vyanzo mbalimbali rasmi idadi ya vifo nchini Msumbiji, Zimbabwe na Malawi inaelezwa kuwa zaidi ya 700. Siku ya Jumanne, lilitolewa ombi la dola miliomi 282 za Kimarekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako