• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Somalia afanya mabadiliko jeshini kukabiliana na hali ya kutokuwa na usalama nchini

    (GMT+08:00) 2019-03-31 17:11:17

    Rais wa Somalia Mohamed Farmajo jana aliwahamisha makamanda wa juu wa jeshi kwenye mabadiliko madogo ikiwa ni sehemu ya hatua ya kukabiliana na hali ya kutokuwa na usalama inayoongzeka nchini humo.

    Kwenye mabadiliko hayo, Abdi Mohamed Hassan aliyekuwa mwambata wa jeshi kwenye ubalozi wa Somalia nchini Saudi Arabia ameteuliwa kuwa naibu kamanda mpya wa jeshi la taifa la Somalia SNA. Hassan anachukua nafasi ya Odawaa Yusuf Rageh aliyeteuliwa kuwa kamanda mpya wa vikosi vya askari wa miguu. Naye Abdirashid Abdullahi Shire ametajwa kuwa naibu kamanda mpya wa vikosi vya askari wa miguu wakati mkuu wa jeshi la wanamaji Abbas Amin Ali ameteuliwa kuwa kamanda mpya wa jeshi la wanamaji, akichukua nafasi ya mkuu wa jeshi la wanamaji aliyefukuzwa kazi Disemba 2018 baada ya kuwa madarakani kwa miezi minne tu. Mabadiliko hayo yamekuja kufuatia kuongezeka kwa mashambulizi ya kigaidi nchini humo ambayo yanadaiwa kusababishwa na kundi la al Shabab.

    Habari nyingine zinasema Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amemteua George Conway kutoka Canada kuwa kaimu naibu mwakilishi maalumu wa Kikosi cha Kutoa Misaada cha Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako