• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuongeza hali ya kuaminiana na kuzidisha ushirikiano ni muhimu kwa China na Marekani

    (GMT+08:00) 2019-03-31 17:11:52

    Baraza la China la Michigan limefanyika jana katika chuo cha biashara cha Ross cha chuo kikuu cha Michigan. Wataalamu wa China na Marekani wanaohudhuria baraza hilo wanaona kuwa, China na Marekani zina mambo mengi yenye maslahi ya pamoja, zinapaswa kuongeza hali ya kuaminiana na kuzidisha ushirikiano. Hii siyo tu itanufaisha nchi hizo mbili na watu wake, bali pia ni muhimu kwa amani na ustawi wa dunia.

    Balozi mdogo wa China mjini Chicago Bw. Zhao Jian amesema, miaka 40 iliyopita tangu China na Marekani kuanzisha uhusiano wa kibalozi, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umebadilika sana, lakini umuhimu wa uhusiano kati ya China na Marekani kwa maslahi ya wananchi wa pande mbili hasa watu wa dunia nzima haubadiliki, na ukweli kuhusu maslahi ya pamoja ya China na Marekani ni mkubwa kuliko tofauti hivyo haubadiliki, hali ya msingi ya ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Marekani haibadiliki, njia ya kushirikiana na nchi nyingine ya kuheshimiana, kuaminiana haibadiliki, na matumaini ya watu wa nchi mbili ya kuongeza maelewano, urafiki na ushirikiano pia hayabadiliki.

    Profesa wa elimu ya siasa wa chuo kikuu cha Michigan Ronald Inglehart amesema, kauli kuhusu maendeleo ya kasi ya China yametishia Marekani si sahihi, China kuendelea kujiendeleza na kupanua kufungua mlango kumeleta fursa nyingi zaidi za ushirikiano kwa Marekani na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako