• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China atoa salamu za pongezi kwa mkutano wa kamati ya viongozi wa umoja wa nchi za kiarabu

    (GMT+08:00) 2019-03-31 17:32:06

    Rais Xi Jinping wa China leo ametoa salamu za pongezi kwa rais Beji Caid Essebsi wa Tunisia ambaye ni mwenyekiti wa zamu wa mkutano wa 30 wa kamati ya viongozi wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, pia akipongeza kufunguliwa kwa mkutano huo.

    Rais Xi alisema kuwa, Umoja wa Nchi za Kiarabu unafanya juhudi katika kuhimiza amani, utulivu na maendeleo ya eneo la Mashariki ya Kati, na kupendekeza kutatua masuala nyeti kwa njia ya kisiasa, na kufanya juhudi kubwa ya kutimiza mashirikiano na kujitegemea kwa nchi za kiarabu. Ameeleza kuwa China inapenda kushirikiana na nchi za kiarabu kufanya juhudi kwa pamoja, kuzidisha hali ya kuaminiana ya kimkakati, kuhimiza ushirikiano halisi, kuongeza maingiliano ya watu, kutekeleza azimio la kujenga kwa pamoja pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia moja, kufungua mustakabali mzuri zaidi wa uhusiano wa kiwenzi na kimkakati kati ya China na nchi za kiarabu, na kutoa mchango katika kuhimiza kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako